Powered By Blogger

Alhamisi, 11 Aprili 2024

Waziri Jafo akutana na Balozi wa Denmark

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mhe. Mette NΓΈrgaard Dissing-Spandet jijini Dodoma leo Machi 18, 2026.
 
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Dkt. Jafo amesema Tanzania inathamini ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili na inatarajia kuendelea kushirikiana zaidi katika hifadhi ya mazingira.
 
Amesema kuwa Tanzania inashirikiana na Denmark katika kusukuma mbele ajenda ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ambayo itasaidia katika kupunguza kasi ya ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.
 
Kupitia ajenda hiyo amemtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa ameonesha dhamira ya dhati ya kuhakikisha asilimia kubwa ya wanawake wa Tanzania na Afrika kwa ujumla wanatumia nishati safi ya kupikia.
 
Dkt. Jafo amesema kuwa katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tanianchi (COP28) uliofanyika Dubai, Falme za Kiarabu, Rais Dkt. Samia alizindua Mradi wa Nishati Safi ya kupikia itakayowasaidia wanawake barani Afrika.
 
Kutokana na umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, Waziri Dkt. Jafo amesisitiza ni wakati sasa Tanzania inahitaji kuwabadilisha wananchi kuachana na matumizi ya kuni na mkaa na kuanza kutumia nishati safi ya kupikia.
 
Ameongeza kwa kuwashukuru wawekezaji wa nishati safi ya kupikia hususan gesi kwa kuunga mkono Serikali kwa kutoa mitungi ya gesi kwa taasisi mbalimbali zinazolisha watu zaidi ya mia moja.
 
Halikadhalika, Dkt. Jafo amesema Tanzania inatekeleza mikakati mbalimbali ya kukabiliana na athari za uharibifu wa mazingira ambapo ilizindua Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021, Mpango Kabambe wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022-2032).
 
Kwa upande wake Mhe. Balozi Dissing-Spandet amemuhakikishia Waziri Jafo kuwa nchi yake itaendeleza ushirikiano wake kwa Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo ya mazingira.
 

Ijumaa, 9 Februari 2024

THUWAIBA "CHUBELLA" AKUTANA NA ZUIO LA SMZ KWENYE MICHEZO Na FINE NONO.


Kwenye Hali ya kushtua na kusikitisha Sana Mwanaharakati, Mwanamichezo na Mpenzi wa soka Zanzibar Ndugu Thuwaiba Aboud Muhidin amekutana na ZUWIO LA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MICHEZO NA KULIPA FINE.

Maamuzi haya ya Baraza la MICHEZO yametolewa kutokana chapisho la tarehe 6/2/2024 
Chanzo cha #WambajeUpdates kimekutana na malalamiko na upokeaji wa maamuzi haya kutoka Kwa Ndugu Chubeilah na kusema haya "...Tangu niko mdg mpk leo hii jina analoniita baba angu ni JIKE LA SIMBA 
Wapendwa wangu hakuna chochote kinachoniumiza kwenye iyo barua niko sawa kuliko nlivokua sawa nyakati zilizopita
KILA KIZA KINAPOKUA KIKUBWA BAC JUA KUNA PAMBAZUKA✌🏽..."

Alhamisi, 8 Februari 2024

NILAUMU MACHO YANGU LYRICS




Moyo umesalitika, na sababu macho yangu, Tena nnafedheheka, kupenda kitu si changu, Mwisho ntaadhirika, kupoteza pendo langu, Nilaumu macho yangu, au moyo nambieni.

Umeuliza suali, jawabu nakuletea,
Uamuzi wa halali, hukumu iso hatia,
Itakuwa ni muhali, kimoja kukionea,
Laumu vyote viwili, usilaumu kimoja.

Na moyo hausikii, umeshitadi wenzangu, Wala haujizuwii, ukaficha siri yangu, Bali wafanya bidii, upoteze roho yangu, Nilaumu macho yangu, au moyo nambieni.

Jicho hufanya idili, mzuri kumvumbua,
Na moyo bila suali, apendae huchagua,
Nawe ufurahi kweli, mapenzi kuyachukuwa, Laumu vyote viwili, usilaumu kimoja.

Macho yangu yamenena, lawama hizi si zangu, Mimi kweli nimeona, hazifumba mboni zangu, Moyo subira hauna, niutendeje wenzangu, Nilaumu macho yangu, au moyo nambieni.

Macho ndio ya awali, matatani kukutia,
Moyo ukawa wa pili, lawamani kuingia,
Moyo hauna akili, jicho halina pazia,
Laumu vyote viwili usilaumu kimoja.

Wa kumshauri sina, nikampa siri yangu,
Yareti angeniona, akajua hali yangu,
Nakufa huku naona, na sababu macho yangu, Nilaumu macho yangu, au moyo nambieni.

Who’s gonna win the π€π…π‚πŽπ? πŸ†πŸŒ

…who’s gonna win the π€π…π‚πŽπ? πŸ†πŸŒ



KOROSHO TANI ZA KUTOSHA ZIPO STOO

#BIASHARA Viongozi wilayani Nachingwea Mkoa wa Lindi wamekiri kuwepo kwa shehena ya korosho ambazo mpaka sasa hazijauzika ambapo wakulima wameombwa kuwa na subra kwa kipindi hiki ambacho wanunuzi wanaendelea kujitokeza kidogokidogo.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wa Chama cha MsingI cha Nambambo AMCOS, Bi SEKERA JACOB ambaye ni mhasibu wa chama hicho amesema, wakulima wamepata changamoto ya kutolipwa hadi sasa ambapo chama chake pekee zaidi ya tani 12 hazijauzwa na hawana uhakika endapo wanunuzi watajitokeza.




Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mohammed Moyo amethibitisha kuwepo kwa korosho tani 51 na kilo 494 ambazo zimebaki kwenye maghala mawili na Serikali imejiridhisha kuwepo kwa korosho hizo huku ikielezwa kuwa kuna wanunuzi ambao wamejitokeza na wamedhamiria kununua korosho zote.

Aidha, Serikali imewashauri wananchi kuwa watulivu wakisubiri kulipwa fedha zao huku wakulima wengine ambao hawajapeleka korosho ghalani wakiomba kuzipeleka kwani uhakika wa kuziuza ni mkubwa. 

WENYE JINSIA TATA WAPATIWA UFUMBUZI MUHIMBILI

Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakishirikiana na Wataalamu kutoka Nchini Ireland na Bahrain, wamewafanyia Watoto 31 upasuaji wa mfumo wa mkojo na haja kubwa ambapo sita kati yao walizaliwa wakiwa na jinsia tata.

Kutokana na hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Mohamed Janabi ameshauri Wazazi kuona umuhimu wa kujifungulia kwenye vituo vya afya ili Watoto wakizaliwa waweze kufanyiwa uchunguzi wa kina na kugundulika mapema ili isaidie kutibiwa mapema “Jamii iache tabia ya kuwanyooshea Watoto vidole pale wanaponekana wanafanya tabia zisizo za kawaida badala yake wawalete hospitali ili wafanyiwe uchunguzi na kupatiwa msaada”



Naye Daktari Bingwa Mbobezi wa Upasuaji wa Watoto MNH Dkt. Petronilla Ngila amesema Mtoto anaweza akazaliwa akaonekana kuwa na maumbile ya kiume lakini kwa ndani anaweza kuwa na homoni na endapo akiendelea kulelewa kama Mtoto wa kiume akifikia kipindi cha balehe ataanza kuingia kwenye siku zake kama mtoto wa kike.

Akizungumzia ukubwa wa tatizo Daktari Bingwa Bobezi wa Upasuaji Mfumo wa Mkojo na Upandikizaji wa Figo Dkt. Gabriel Mtaturu amefafanua kuwa kati ya Watoto elfu tano wanaozaliwa mmoja ana jinsia tata na kati ya Watoto 300 wanaozaliwa mmoja anazaliwa akiwa na jinsia zilizoungana.


“Watoto waliofanyiwa upasuaji walikuwa katika makundi manne ambapo baadhi walikuwa na jinsia tata,wengine walikuwa na maumbile ya kike ila ndani walikuwa na maumbile ya kiume, mmoja alikuwa na sehemu mbili za kutolea haja ndogo na mwingine alikuwa wa kike ila hana sehemu za siri hivyo walimfanyia upasuaji rekebishi na kumtengenezea maumbile ya kike” 

#WambajeUpdates

Teknolojia Itumike Kutatua Changamoto Ya Ajira Afrika

 

Teknolojia Itumike Kutatua Changamoto Ya Ajira Afrika


Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. Phillip Mpango akizungumza na wadau mbali mbali wa ajira wakati akifungua mkutano wa saba wa washirika wa Kijamii wa Afrika ( ASP). Mkutano huo uulioandaliwa na Chama cha waajiri Tanzania ( ATE) umeanza leo Februari 7,2024 katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam na unatarajiwa kumalizika kesho Februari 8,2024

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
MAKAMU wa Rais Dkt. Phillip Mpango amezitaka nchi za Afrika kuchukua hatua za kutumia maendeleo ya teknolojia ili kukabiliana na ukosefu wa ajira pamoja na ka kuchochea uzalishaji na ukuaji wa uchumi barani humo.

Dkt.Mpango ametoa wito huo leo, Frebuari 6, 2024, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 7 wa Washirika wa Kijamii wa Afrika, uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amewashauri wajumbe wa mkutano kuitazama teknolojia ya akili bandia (AI) kama fursa na kwamba wasihofie.

"Katika eneo la maendeleo ya teknolojia, kunadhaniwa kwamba nafasi za ajira zitaathiriwa na AI. Pamoja na kuwa na dhana hiyo lakini teknolojia hiyo itatengeneza ajira mpya hasa zile zinazohitaji ujuzi wa kiufundi,” amesema

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 50 barani Afrika DKt. Mpango amesema kuwa muhimu kuendeshwe mafunzo yatakayoendana na mabadiliko ya teknolojia na kubaini sekta zenye fursa nyingi za ajira.

"Sekta ambazo akili bandia zinaweza kuongeza ajira ni kilimo ambapo AI inaweza kukuza utafiti wa kilimo kwa kubaini aina ya mbegu bora itakayomudu mabadiliko ya hali ya hewa " alisema.


Akizungumza nje Mkutano huo , Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Suzan Ndomba amesema mkutano huo utajikita katika masuala ya uzalishaji wa ajira kwa mada tofauti na kuja na mapendekezo.

Kwa upande wake, Roberto Suarez Santos, Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Waajiri (IOE) ameema, mkutano huo unatoa fursa ya kuunda suluhisho na mbinu za pamoja za kutatua changamoto za ajira kwa vijana na kwa ukosefu wa utulivu wa kijamii.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Said Wamba, amesema wakiwa wadau shirika lao linatarajia kujadili namna ya kuendeleza mijadala na midahalo yenye nia ya kuboresha uhusiano kati ya chama na waajiri kwa sababu ajira inamnufaisha kila mtu akiwemo mustakabali wa sekta ya ajira.

DKT. SAMIA ASISITIZA UCHAGUZI UTAKUWA WA DEMOKRASIA, WA HAKI, SHERIA NA UTAWALA BORA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema haki, demokrasia, sheria na utawala bora utadumishwa kwa watu wote wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.


Rais Samia amesema hayo leo katika sherehe za mwaka mpya 2024 (Diplomatic Sherry Party) kwa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa zilizofanyika Ikulu.

Aidha, Rais Samia amesema ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, Kikosi Kazi huru cha kupitia na kushauri mageuzi muhimu katika mfumo wa siasa kiliundwa ambapo kiliwasilisha ripoti yake mwaka 2023.



Rais Samia pia amesema mapendekezo mengi ya Kikosi Kazi yaliyopokelewa na serikali na wadau wote yalihusu kuongeza uwazi katika michakato ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.

Vile vile, Rais Samia amesema masuala machache hayakupokelewa moja kwa moja ambayo yalikuwa kinyume na katiba hivyo yanaweza kuchukuliwa wakati wa mchakato wa marekebisho ya katiba.



Rais Samia amesema serikali itaendeleza ushirikiano na balozi hizo kwa mujibu wa katiba, tunu za kitaifa, usawa, umoja na mshikamano wa kitaifa huku akiwataka mabalozi hao kutokuingilia uchaguzi na kuzingatia mila, kanuni na maadili ya kidiplomasia.



Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema Tanzania inasikitishwa na vita vinavyoendelea Palestina na kusababisha mauaji ya watoto na raia wasio na hatia na inaunga mkono usuluhishi kati ya Palestina na Israeli kwa kutoa wito wa kusitishwa mapigano na kupatiwa misaada ya kibinadamu.


Jumatano, 7 Februari 2024

Timu ya DRC kuhimiza Amani kwenye Nusu Fainali AFCON 2023

Timu ya Taifa ya DRC inakwenda kuutumia mchezo wa Nusu fainali ya Mataifa ya Afrika AFCON kutuma ujumbe na kutoa pole kwa waathiriwa wa mapigano Kaskazini mwa nchi hiyo.

Wamesema kuwa hawatavaa jezi kwa ajili ya kupata ushindi bali kutuma ujumbe lakini pia na kutoa pole kwa wahanga wa mapigano lakini pia na kuomba maridhiano kati ya Serikali na Waasi.




Nahodha wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Chancel Mbemba amechapisha ujumbe unaosema kuwa “Naomba mara kwa mara nchi yangu iweze kurejea katika hali ya utulivu na watu wapate amani”.

Mashariki mwa DR Congo mapigano yameendelea kuripotiwa kati ya jeshi la DRC na waasi wa M23 na kusababisha maaelfu ya watu kuyakimbia makazi yao huku wengine wakiuawa.



DRC inatarajia kukipiga na Ivory Coast kwenye Nusu fainali Februari 7, 2024 ikiwania kutwaa kombe hilo mara mbili baada ya kulibeba miaka 50 iliyopita.

#KitengeSports

VYOMBO VYA HABARI MSIWABAGUE WANA SIASA; WAPENI NAFASI WOTE

Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye amesema Serikali ya awamu ya sita haijawahi na haina mpango wa kuminya uhuru wa Vyombo vya Habari ambapo amevitaka Vyombo hivyo kuwapa nafasi Wanasiasa wote bila kujali tofauti ya Vyama vyao.



Akiongea Jijini Dodoma leo, Nape amesema “Serikali imeona kupitia Vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kuhusu Wasafi FM kuzuia mahojiano kati ya Tundu Lissu na Radio hiyo katika kipindi chao cha Good Morning na maelezo yaliyotolewa yalisema wamezuia kwa maelekezo kutoka juu lakini baadaye nimeona Lissu mwenyewe akisema kwamba amepewa taarifa kwamba ilikuwa ni mkanganyiko wa ndani wa Wasafi”

“Serikali inatoa taarifa kwamba toka Rais Dkt. Samia Suluhu ameingia madarakani ameimarisha uhuru wa Vyombo vya Habari na Demokrasia, kilichotokea leo kimetusikitisha hasa kauli kuwa ni maelekezo kutoka juu, Serikali ya Rais Samia haijafanya na haina mpango, tuondokane na hofu ya kujifungia sehemu na kuwa na visingizio kwamba kuna maagizo, kuna Serikali inafanya hivi hapana”



“Nitoe wito kwa Wanahabari, timizeni wajibu wenu kwa kufuata sheria, Serikali haina mpango wa kuingilia uhuru wa Wanahabari kutimiza majukumu yao, kama kuna mahali Watu wanaamua kutumia content yoyote wafanye kwa kufuata sheria lakini hakuna Kiongozi yeyote wa Serikali ambaye ana mpango wa kuingilia uhuru wa Vyomvo vyetu vya habari kutimiza majukumu yao”

“Natoa wito kwa Wasafi hiki kipindi walichokiahirisha wakifanye, Vyombo vyote vya Habari wapeni uwanja sawa Wanasiasa watimize majukumu yao, Mtu akisemwa, wa upande wa pili apewe nafasi ya kujieleza ndio namna ambavyo tutaendesha siasa za Nchi yetu, Rais Samia kupitia 4R zake ameelekeza, tuvumiliane, tufanye maridhiano, na haya ndiyo mambo ya kufanya, na Rais ameonesha kwa mfano, juzi CHADEMA wameomba maandamano wameruhusiwa”




“Vyombo vinavyisimamia maeneo hayo tuvipe Vyombo vya Habari, tusiwaingilie, na yoyote anayefanya haya anamuhujumu Mh. Rais , tusiichafue Serikali kwasababu ya visingizio, tangu Rais Samia aingie hatuna maelekezo tunayoyatoa kwa Vyombo vya Habari, tumewapa uhuru mtimize wajibu wenu, mfanye kazi zenu kwa uhuru, sasa tusitafute visingizio ambavyo havina sababu, Serikali hatuna sababu ya kuingilia uhuru wa Vyombo vya Habari, nampa pole Mjomba wangu Lissu kwa kadhia aliyoipata asubuhi, narudia wapeni uwanja sawa Wanasiasa waongee kwa hoja na hasa tunapoelekea kipindi cha uchaguzi”
#MillardAyoUPDATES

MALARIA BADO NI GUMZO ZANZIBAR

Afisa wa Afya ya Jamii Wizara ya Afya Mwinyi Khamis amesema licha ya juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali za kupambana na ugonjwa wa malaria bado jamii haipo tayari kuunga mkono juhudi  hizo jambo ambalo linapelekea kuongezeka  kwa  ugonjwa huo visiwani Zanzibar.




Akizungumzia hali ya malaria nchini katika mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari  juu ya magonjwa ya mripuko yakiwemo malaria, macho na matumbo huko kitengo cha elimu ya afya Sogea amesema takwimu za wizara ya afya zinaonyesha kuwa ugonjwa huo umeongezeka takribani kwa wilaya zote za Zanzibar na kuwaathiri zaidi  wanaume wenye umri kati ya miaka  15 hadi 45.

“wanaoathirika zaidi  kwa ugonjwa huu ni wanaume ikiwemo  waendesha boda boda, wajenzi wa usiku, wanakwenda kumbi za starehe usiku pamoja na watazamaji mpira nyakati za usiku”, alifahamisha.

Alieleza kuwa kutokana na takwimu hizo  wilaya ya mjini inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa  ya wagonjwa  ikifuatiwa na wilaya ya magharibi B.

Amesema hali ya ongezeko la ugonjwa huo ni kutokana  na jamii kutokutumia njia za kujikinga ikiwemo kulala kwenye vyandarua ,kuchelewa kufika vituo vya afya kwa wenye dalili  za ugonjwa , kuwepo kwa mazalia ya mbu pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.

Afisa huyo aliitaka jamii kudumisha usafi katika maeneo na kufika katika vituo vya afya ndani ya masaa 24 mara wanapopata dalili za homa ili kupata matibabu katika wakati sahihi.   



Aidha amesema  wizara kupitia kitengo cha elimu ya afya  inaendelea kudhibiti ugonjwa wa malaria  kwa  kutoa elimu ya afya kwa jamii, tiba kwa wale waliogundulika kuwa na vimelea vya malaria, upigaji wa dawa majumbani kwa maeneo yaliathiriwa zaidi, kutoa dawa na kuichunguza damu jamii iliyo karibu na  mgonjwa, pamoja na kutia viatilifu kwenye madimbwi ya maji.

Akizungumzia hali ya macho mekundu, Mratibu wa huduma za Afya ya Msingi na matibabu ya macho  Dkt Rajab Mohammed  Hilal amesema jumla ya watu 12860 wamepatiwa matibabu katika vituo mbalimbali vya afya Zanzibar na kwa  sasa hali ya ugonjwa huo imepungua.

Aidha alieleza kuwa jumla ya wagonjwa 5 walilazalwa katika  hospital ya rufaa ya  Mnazi mmoja baada ya kutumia dawa ambazo sio sahihi katika  kutibia ugonjwa huo akiwemo mtoto wa  miaka  11 ambapo walipoteza uoni wao.

Mratibu huyo aliisisitiza jamii kuacha utamaduni wa kutumia dawa za kienyeji na kufika katika vituo vya afya ili kupata matibabu sahihi.

“Baadhi ya takwimu kwa wagonjwa waliotibiwa  katika vituo vyetu  kwa Zanzibar ni pamoja na wagonjwa 1,459 katika kitengo cha matibabu ya macho Hospitali ya  Mnazi mmoja, 3,432 Kwamtipura, 2,316 Mpendae, 22 Chake chake,1,320 Kivunge, 993 Wete,25 Shungi, Kambini kichokochwe  65, 54 Wesha,  65Wingwi,   100 Pujini,  480 Micheweni  ,na 660 Mkoani .” alieleza mratibu huyo


Akiwasilisha mada ya mazingira Meneja wa Kitengo cha Elimu ya Afya Zanzibar  Bakari Hamad Magarawa amesema hali ya uchafu wa mazingira inachangia ongezeko la magonjwa ya mripuko ikiwemo malaria na kipindupindu na kuitaka jamii kudumisha usafi katika maeneo yao pamoja na kuzingatia maelezo ya kitaalamu ili kujiepusha na   magonjwa hayo.

Hata hivyo aliwasisitiza  waandishi waliopatiwa mafunzo hayo kuifikisha elimu  kwa jamii  ili kujua hali halisi juu ya Magonjwa hayo na kuweza  kujikinga.

Jumla ya watu 11 wamefariki kutokana na  ugonjwa  wa maleria kuanzia Januari 1 hadi januari 26 mwaka huu.

RAIS DK.MWINYI ATOA AGIZO KUANZA KAZI MAHKAMA YA RUSHWA ZANZIBAR



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameagiza taasisi zinazo husika na sheria kukamilisha mchakato wa utungaji wa sheria ili kuanza kazi kwa Mahkama Maalum ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi kwa mwaka huu.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Sheria Zanzibar katika viwanja vya Mahkama kuu Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 07 Februari 2024.




Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuimarisha mhimili wa Mahkama na Taasisi zote za Sheria ili ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi, hatua hizo ikiwemo ujenzi wa majengo saba (7) ya Mahkama katika Mikoa na Wilaya Zanzibar, kuongeza idadi ya Majaji, Mahakimu na Makadhi pamoja na  kuboresha maslahi  kwa Majaji, Mahakimu, Makadhi na watumishi wengine wa Taasisi za sheria ili kuongeza ufanisi. 

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amesema ustawi bora wa wananchi utategemea kuwepo kwa misingi imara ya kuheshimu haki za binadamu, utawala bora, uhuru wa Mahkama pamoja na sheria madhubuti zinazoilinda jamii dhidi ya aina zote za unyanyasaji. 

Vilevile Rais Dk.Mwinyi ameipongeza Mahkama ya Zanzibar kwa kuanza  mchakato wa kuboresha mfumo wa kieletroniki wa usikilizaji wa mashauri kwa msaada wa kitalaamu kutoka Mahakama ya Tanzania.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amezindua mpango mkakati wa miaka mitano wa Mahkama (2024-2029) na kukabidhiwa ripoti ya utendaji kazi wa Mahkama ya mwaka 2023.

UTEUZI SMT




Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Thomas Nestory Bwana kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Kabla ya uteuzi huu Dkt. Bwana alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais na anachukua nafasi ya Dkt. Geofrey Mkamilo ambaye amemaliza muda wake.

Amemteua pia aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ambapo Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba atapangiwa kazi nyingine.

Rais Samia amemteua pia Dkt. Bill Kiwia kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) akichukua nafasi ya Badru ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF.

VAZI LA TAIFA LA TANZANIA 2024 LITAPATIKANWA.

Serikali imesema Kamati ya kuratibu upatikanaji wa vazi la Taifa imekusanya maoni kutoka kwa Wadau na Wananchi 2,452 katika Mikoa yote Tanzania na kwa sasa itakutana ili kuwashindanisha Wabunifu wa mavazi (Designers) ili watakaokuwa Washindi  mavazi yao ndiyo yatakayopendekezwa kuwa vazi la Taifa.



Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ( @MwanaFA ) ametoa kauli hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Malinyi, Antipas Mgungusi aliyehoji kwamba ni lini Tanzania itapata vazi la Taifa? ambapo Naibu Waziri alimjibu kwa kusema kabla mwaka huu wa 2024 haujaisha vazi la Taifa litakua limepatikana.

“Tumeamua kutumia njia hii ili kuharakisha mchakato na kupunguza uhitaji wa fedha nyingi za uratibu wa upatikanaji wa vazi la Taifa, Kamati hii sio ya siri ilitangazwa mwaka 2022  na ina Mwenyekiti, Makamu na Wajumbe tisa akiwemo Masoud Ally Kipanya, Mrisho Mpoto, Khadija Mwanamboka na wengineo na ilishakamilisha kazi yake na jambo limerudi Wizarani ili kukamilisha mchakato huu, mwaka huu 2024 hautokwisha kabla hatujapata vazi la Taifa” ——— Naibu Waziri Mwinjuma. 

Qarim Zam — How the photographer captures the heart of his home, Zanzibar

 



Stone Town is the old port of Zanzibar City, Tanzania, and it’s teeming with history and heritage that brings in visitors from around the world. 

So, who better to introduce you to its narrow alleys and turquoise waters than someone born and raised there? 

Stone Town local and photographer Qarim Zam tells writer Alix-Rose Cowie how he goes about capturing its everyday magic.

For many documentary photographers, it’s the thrill of visiting somewhere new or far-flung that gets their shutter clicking; bringing home stories from different time zones, and meeting people who broaden their perspectives and portfolios. But it’s a gift to be able to look at a place you’ve known your whole life, seeing people who could be family, on streets so familiar you could walk them blindfolded, and thinking, “there’s something valuable here worth sharing.” Though, it probably helps when your home is a beautiful island off the coast of east Africa. Mukrim Qarim Zam is an aspiring documentary photographer—he calls it a hobby for now—who lives in Stone Town, a historic district of Zanzibar, and lives by the motto: Show your world, to the world.

Wherever he shares his photography, Zam drops his first name and goes by Qarim, the name of his father who he lost five years ago when he was just 20 years old; it was around the same time that he started taking photos. He doesn’t own a camera so all of his gorgeous slices of life on the island are captured using his iPhone, the tool that’s most accessible to him. When it comes to the act of taking a picture—assessing the light, angling the shot and framing the subject—Zam is self-taught. It’s something that comes to him intuitively. Editing was the area he sought instruction; he learned from established Tanzanian photographer and Lightroom ambassador Sam Vox when he’d visit Zanzibar for his own projects, and utilized his open-source presets to brighten or warm his pictures.

Alcohol shortage hits Zanzibar Tourism Sector

 The spice islands of Zanzibar are facing a shortage of alcohol which threatens the tourism sector of one of Africa's top travel destinations.

Tourism generates about 90% of the Tanzanian archipelago's foreign revenue.

Prices of beer have shot up by almost 100% after the supply chain was disrupted by a sudden change of importers.




The islands' tourism minister resigned recently citing poor work conditions.

However, some have linked his resignation to the issues with alcohol supplies.

Known for their stunning sandy beaches and rich cultural heritage, the Indian Ocean islands are popular with tourists from around the world.

Last year, Zanzibar was ranked among the 10 best travel destinations in Africa by several tour magazines.

But hoteliers now warn that the problems over alcohol supply might make the island lose its tourism shine.

Several tourist hotels along the Matemwa beaches in the north of Zanzibar's main island are only serving soft drinks and people in that area say they have to go to the main city, Stone Town, for alcohol.

Mr Mshenga's business selling beer and sea food has been badly hit.

"We are running short of beer at my bar, and I just have a stock of soft drinks," he told the reporter. "The government has to take action. It is the high season now, it is very hot and these tourists need joy, they need cold beer on these beaches."




An American tourist, who did not want to be named, said: "I love Zanzibar and its beaches. The people are amazing and only challenge I feel now is I can't get hard liquor. I want to have spirits or even whisky but nothing is found in the hotel - they instead advised me to order it from Stone Town."

The local manufacture of alcohol is banned in Zanzibar, whose population is largely Muslim.


Most of the alcohol sold on the islands comes from mainland Tanzania, while some is imported from South Africa.

The initial shortage early this year began when the Zanzibar Liquor Control Board (ZLCB) delayed renewed permits for the three established importers - One Stop, Scotch Store, and ZMMI.

It is not clear why the licences of the three firms, which had supplied alcohol to the island for more than two decades, were not renewed.

For alcohol importers to get licensed, they must be Zanzibari-born residents with a clean tax record, a warehouse, and a delivery vehicle.

Additionally, importers must also pay a $12,000 (£10,000) annual fee to the regulatory board.




Last month, ZLCB granted licences to three new companies - Kifaru, Bevko and Zanzi Imports - but hoteliers say they are still struggling to meet the demand.

The new firms are reportedly entangled in a lengthy vetting process amid reports that some non-Zanzibaris are involved in the operations of the companies in contravention of the law.

The situation has been complicated further after the three previous licence holders filed appeals, asking the government to renew their liquor import permits.

Zanzibar's liquor stores are struggling to keep shelves stocked.


"There is an alcohol shortage in Zanzibar and we've already informed authorities about the tourism sector's situation," Rahim Mbarouk, chairman of the Zanzibar Tourism Investment Association, told the reporter.

The price of beer has gone up from 2,500 shillings ($1; £0.80) to 5,000 shillings, according to Neema Meena, a frequent traveller to Zanzibar from mainland Tanzania.

Some popular alcohol brands, like Safari, are said to be completely unavailable.

"This shortage hits hard," Frank John Kahamu, secretary at the Amani Alcohol Merchants Union, told privately-owned The Citizen website.

Mr Kahamu said more than 3,000 workers could lose their jobs if the situation continued.

"We can't keep paying wages with empty shelves."

ZLCB chairperson Juma Chum declined to respond when the reporter reached out for comment.

But Issa Mahfoudh Haji, a senior official in the Ministry of State responsible for the ZLCB, told state media: "We have heard about the complaints and we need to find details about the controversy."

Simai Mohammed Said resigned as tourism minister last week, citing "unfavourable and disruptive working conditions".

His resignation has been linked to a recent press conference where he publicly accused the ZLCB of mismanaging the liquor industry.

"If we fail to plan, including having enough stock of alcoholic beverages, we frustrate our visitors," he said, according to state media.

But while swearing in the new tourism minister on Thursday, Zanzibar President Hussein Mwinyi suggested Mr Said had a conflict of interest.

Reports link one of Mr Said's relatives to one company whose licence was not renewed.

"If you have a bar, and you find out authorities have not given access to alcohol to your bar, then be transparent and tell the public that there is conflict of interest," President Mwinyi said, referring to Mr Said.


The crisis comes amid soaring tourist arrivals in the semi-autonomous Tanzanian islands.

They witnessed a 16% surge in international visitors last year, welcoming a record more than 630,000 tourists, according to the annual tourism report.

The tourist upsurge was due to significant increases of arrivals from India and Russia, the report said.

Sauti za Busara festival 2024 line-up

The organizers of Sauti za Busara in Zanzibar have announced the artist line-up for the festival’s 21st edition in Stone Town from 9 to 11 February 2024.



The line-up features a diverse array of renowned and emerging musicians hailing from various corners of the African continent and the diaspora. 

“This selection is a musical journey across Africa, spanning the vibrant rhythms of the East to the soulful melodies of the North, the energetic beats of the South and the captivating sounds of the West,” the organisers said.

The 2024 festival will also see Lorenz Herrmann in charge as the new managing director after taking over from founder and CEO Yusuf Mahmoud who retired after 20 years at the helm in July. The theme for the 21st edition is Moving Diversity.

“[As we celebrate] live music from across Africa and beyond, once again the spotlight shines brightly on women artists and young and emerging talents with unique sounds, powerful messages, excitement and energy on stage,” Sauti za Busara festival director Journey Ramadhan said.

“For three days two stages inside the Old Fort (Ngome Kongwe) and one free stage in the Forodhani Gardens, just outside the Old Fort, will feature thrilling and unique performances. Visitors to our website can watch videos and learn about all the groups that will be performing next February.”

Below is the Sauti za Busara 2024 artist line-up:

SOMO LA BURE (I)






Vijana Kuna mambo Mnaweza kufanya kwa pamoja na mkajikuta mmetoka.

Mnajitafuta vijana wanne au watano wenye career tofauti ila kwa combination. Mfno;-

1. Graphics Designer
2. Photo & Videographer
3. Motions Designer
4. Social Media Manager

Mnaji-organise na kufungua ofisi yenu.

Hii sio kampuni, Bali ni shared ofisi. Kwa maana kila mmoja anakuwa na meza yake aliyonunua yeye na kila mtu anakuwa na mashine yake na vifaa vyake vyote mwenyewe. 

Ila Kuna vitu mnashare. Mfano; Kodi ya pango/nyumba/eneo la kazi, umeme, Internet, decoration ya ofisi, gharama nyengine zote za kuendesha Ofisi/Eneo la kazi.

Ofisi hii Mnaweza kumpa mtu mmoja dhamana ya kutumia TIN yake/Leseni/ZRA (kwa Zanzibar), kisha mkachangiana katika kulipia mapato pamoja na Leseni ili msisumbuliwe.

MNAFANYAJE KAZI?

1. Kila mtu ana wateja wake. Lakini wateja hawa hupenda zaidi kuhudumiwa ofisini kuliko kwenye simu ili wapate kujuamini zaidi. Hivyo kila mmoja ataleta mteja wake pale.

2. Kila mtu atumie social media Account yake na njia zake Mbadala kujitangaza. Na apatapo wateja wakija ofisini, automatically anakuwa mteja wenu wote.

3. Mmoja wenu akipata kazi ambayo kuna mtu anaweza kuifanya humo ndani, basi haiendi mbali.

Hiyo inakuwa kama incubator yenu ambayo mnajipa malengo ya kwamba baada ya muda fulani labda miaka miwili, kila mtu akajitegemee kivyake.

Hii itawasaidia sana kukua kwa kasi zaidi kwa sababu mtashirikiana kwa kupeana kazi.

Sasa ili hili jambo mfanikiwe lazima muwe na mambo yafuatayo.

1. MALENGO MAMOJA
2. NIDHAMU
3. KUTOWEKA USHKAJI
4. UAMINIFU
5. KUTHAMINIANA
6. KUAMINIANA
7. KUSHIRIKIANA
8. KUCHUKULIANA
9. KUSAIDIANA
10. KUTOUPA WIVU NAFASI

Mkifanikiwa hayo mambo, mtaona mambo yenu yakienda vizuri.

Tena kama ofisi yenu ni kubwa tengeni chumba cha kuongea na wateja. Maana wateja wengine hupenda privacy.

Hii itawapunguzia gharama kubwa za kuanzisha ofisi na kuendeleza.

Mfano kupanga ofisi ni
 200,000×6months
=1,200,000.

Then, 1.2M÷4 = 300k

So kila mtu anatafuta 300k kwa miezi 6. Then Kila mwezi mkawe na service charge 30k umeme, internet na ulinzi, taka n.k

Umeona ilivo rahisi?

Vijana mkiwa mnasubiri kupata pesa za ofisi ambapo ni gharama sana, kwanini msichangie afu muingie na kufanya mapambano kwa njia hii?

Then mkishakuwa, kila mtu akapambane zake.

I think it can work fully.

KUTOKA MAGAZETINI LEO

 Kurasa zambele za magazeti ya leo tarehe 7 mwezi wa februari mwaka 2024.


usisitte kutuandikia maoni yako chini kwenye comments.