#BIASHARA Viongozi wilayani Nachingwea Mkoa wa Lindi wamekiri kuwepo kwa shehena ya korosho ambazo mpaka sasa hazijauzika ambapo wakulima wameombwa kuwa na subra kwa kipindi hiki ambacho wanunuzi wanaendelea kujitokeza kidogokidogo.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima wa Chama cha MsingI cha Nambambo AMCOS, Bi SEKERA JACOB ambaye ni mhasibu wa chama hicho amesema, wakulima wamepata changamoto ya kutolipwa hadi sasa ambapo chama chake pekee zaidi ya tani 12 hazijauzwa na hawana uhakika endapo wanunuzi watajitokeza.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mohammed Moyo amethibitisha kuwepo kwa korosho tani 51 na kilo 494 ambazo zimebaki kwenye maghala mawili na Serikali imejiridhisha kuwepo kwa korosho hizo huku ikielezwa kuwa kuna wanunuzi ambao wamejitokeza na wamedhamiria kununua korosho zote.
Aidha, Serikali imewashauri wananchi kuwa watulivu wakisubiri kulipwa fedha zao huku wakulima wengine ambao hawajapeleka korosho ghalani wakiomba kuzipeleka kwani uhakika wa kuziuza ni mkubwa.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni