Powered By Blogger
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo SAUTI YA GAZETI. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo SAUTI YA GAZETI. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 8 Februari 2024

Teknolojia Itumike Kutatua Changamoto Ya Ajira Afrika

 

Teknolojia Itumike Kutatua Changamoto Ya Ajira Afrika


Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. Phillip Mpango akizungumza na wadau mbali mbali wa ajira wakati akifungua mkutano wa saba wa washirika wa Kijamii wa Afrika ( ASP). Mkutano huo uulioandaliwa na Chama cha waajiri Tanzania ( ATE) umeanza leo Februari 7,2024 katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam na unatarajiwa kumalizika kesho Februari 8,2024

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
MAKAMU wa Rais Dkt. Phillip Mpango amezitaka nchi za Afrika kuchukua hatua za kutumia maendeleo ya teknolojia ili kukabiliana na ukosefu wa ajira pamoja na ka kuchochea uzalishaji na ukuaji wa uchumi barani humo.

Dkt.Mpango ametoa wito huo leo, Frebuari 6, 2024, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 7 wa Washirika wa Kijamii wa Afrika, uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amewashauri wajumbe wa mkutano kuitazama teknolojia ya akili bandia (AI) kama fursa na kwamba wasihofie.

"Katika eneo la maendeleo ya teknolojia, kunadhaniwa kwamba nafasi za ajira zitaathiriwa na AI. Pamoja na kuwa na dhana hiyo lakini teknolojia hiyo itatengeneza ajira mpya hasa zile zinazohitaji ujuzi wa kiufundi,” amesema

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 50 barani Afrika DKt. Mpango amesema kuwa muhimu kuendeshwe mafunzo yatakayoendana na mabadiliko ya teknolojia na kubaini sekta zenye fursa nyingi za ajira.

"Sekta ambazo akili bandia zinaweza kuongeza ajira ni kilimo ambapo AI inaweza kukuza utafiti wa kilimo kwa kubaini aina ya mbegu bora itakayomudu mabadiliko ya hali ya hewa " alisema.


Akizungumza nje Mkutano huo , Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Suzan Ndomba amesema mkutano huo utajikita katika masuala ya uzalishaji wa ajira kwa mada tofauti na kuja na mapendekezo.

Kwa upande wake, Roberto Suarez Santos, Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Waajiri (IOE) ameema, mkutano huo unatoa fursa ya kuunda suluhisho na mbinu za pamoja za kutatua changamoto za ajira kwa vijana na kwa ukosefu wa utulivu wa kijamii.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Said Wamba, amesema wakiwa wadau shirika lao linatarajia kujadili namna ya kuendeleza mijadala na midahalo yenye nia ya kuboresha uhusiano kati ya chama na waajiri kwa sababu ajira inamnufaisha kila mtu akiwemo mustakabali wa sekta ya ajira.

DKT. SAMIA ASISITIZA UCHAGUZI UTAKUWA WA DEMOKRASIA, WA HAKI, SHERIA NA UTAWALA BORA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema haki, demokrasia, sheria na utawala bora utadumishwa kwa watu wote wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.


Rais Samia amesema hayo leo katika sherehe za mwaka mpya 2024 (Diplomatic Sherry Party) kwa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa zilizofanyika Ikulu.

Aidha, Rais Samia amesema ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, Kikosi Kazi huru cha kupitia na kushauri mageuzi muhimu katika mfumo wa siasa kiliundwa ambapo kiliwasilisha ripoti yake mwaka 2023.



Rais Samia pia amesema mapendekezo mengi ya Kikosi Kazi yaliyopokelewa na serikali na wadau wote yalihusu kuongeza uwazi katika michakato ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.

Vile vile, Rais Samia amesema masuala machache hayakupokelewa moja kwa moja ambayo yalikuwa kinyume na katiba hivyo yanaweza kuchukuliwa wakati wa mchakato wa marekebisho ya katiba.



Rais Samia amesema serikali itaendeleza ushirikiano na balozi hizo kwa mujibu wa katiba, tunu za kitaifa, usawa, umoja na mshikamano wa kitaifa huku akiwataka mabalozi hao kutokuingilia uchaguzi na kuzingatia mila, kanuni na maadili ya kidiplomasia.



Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema Tanzania inasikitishwa na vita vinavyoendelea Palestina na kusababisha mauaji ya watoto na raia wasio na hatia na inaunga mkono usuluhishi kati ya Palestina na Israeli kwa kutoa wito wa kusitishwa mapigano na kupatiwa misaada ya kibinadamu.


Jumatano, 7 Februari 2024

KUTOKA MAGAZETINI LEO

 Kurasa zambele za magazeti ya leo tarehe 7 mwezi wa februari mwaka 2024.


usisitte kutuandikia maoni yako chini kwenye comments.