Serikali imesema Kamati ya kuratibu upatikanaji wa vazi la Taifa imekusanya maoni kutoka kwa Wadau na Wananchi 2,452 katika Mikoa yote Tanzania na kwa sasa itakutana ili kuwashindanisha Wabunifu wa mavazi (Designers) ili watakaokuwa Washindi mavazi yao ndiyo yatakayopendekezwa kuwa vazi la Taifa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ( @MwanaFA ) ametoa kauli hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Malinyi, Antipas Mgungusi aliyehoji kwamba ni lini Tanzania itapata vazi la Taifa? ambapo Naibu Waziri alimjibu kwa kusema kabla mwaka huu wa 2024 haujaisha vazi la Taifa litakua limepatikana.
“Tumeamua kutumia njia hii ili kuharakisha mchakato na kupunguza uhitaji wa fedha nyingi za uratibu wa upatikanaji wa vazi la Taifa, Kamati hii sio ya siri ilitangazwa mwaka 2022 na ina Mwenyekiti, Makamu na Wajumbe tisa akiwemo Masoud Ally Kipanya, Mrisho Mpoto, Khadija Mwanamboka na wengineo na ilishakamilisha kazi yake na jambo limerudi Wizarani ili kukamilisha mchakato huu, mwaka huu 2024 hautokwisha kabla hatujapata vazi la Taifa” ——— Naibu Waziri Mwinjuma.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni