Powered By Blogger

Jumatano, 7 Februari 2024

SOMO LA BURE (I)






Vijana Kuna mambo Mnaweza kufanya kwa pamoja na mkajikuta mmetoka.

Mnajitafuta vijana wanne au watano wenye career tofauti ila kwa combination. Mfno;-

1. Graphics Designer
2. Photo & Videographer
3. Motions Designer
4. Social Media Manager

Mnaji-organise na kufungua ofisi yenu.

Hii sio kampuni, Bali ni shared ofisi. Kwa maana kila mmoja anakuwa na meza yake aliyonunua yeye na kila mtu anakuwa na mashine yake na vifaa vyake vyote mwenyewe. 

Ila Kuna vitu mnashare. Mfano; Kodi ya pango/nyumba/eneo la kazi, umeme, Internet, decoration ya ofisi, gharama nyengine zote za kuendesha Ofisi/Eneo la kazi.

Ofisi hii Mnaweza kumpa mtu mmoja dhamana ya kutumia TIN yake/Leseni/ZRA (kwa Zanzibar), kisha mkachangiana katika kulipia mapato pamoja na Leseni ili msisumbuliwe.

MNAFANYAJE KAZI?

1. Kila mtu ana wateja wake. Lakini wateja hawa hupenda zaidi kuhudumiwa ofisini kuliko kwenye simu ili wapate kujuamini zaidi. Hivyo kila mmoja ataleta mteja wake pale.

2. Kila mtu atumie social media Account yake na njia zake Mbadala kujitangaza. Na apatapo wateja wakija ofisini, automatically anakuwa mteja wenu wote.

3. Mmoja wenu akipata kazi ambayo kuna mtu anaweza kuifanya humo ndani, basi haiendi mbali.

Hiyo inakuwa kama incubator yenu ambayo mnajipa malengo ya kwamba baada ya muda fulani labda miaka miwili, kila mtu akajitegemee kivyake.

Hii itawasaidia sana kukua kwa kasi zaidi kwa sababu mtashirikiana kwa kupeana kazi.

Sasa ili hili jambo mfanikiwe lazima muwe na mambo yafuatayo.

1. MALENGO MAMOJA
2. NIDHAMU
3. KUTOWEKA USHKAJI
4. UAMINIFU
5. KUTHAMINIANA
6. KUAMINIANA
7. KUSHIRIKIANA
8. KUCHUKULIANA
9. KUSAIDIANA
10. KUTOUPA WIVU NAFASI

Mkifanikiwa hayo mambo, mtaona mambo yenu yakienda vizuri.

Tena kama ofisi yenu ni kubwa tengeni chumba cha kuongea na wateja. Maana wateja wengine hupenda privacy.

Hii itawapunguzia gharama kubwa za kuanzisha ofisi na kuendeleza.

Mfano kupanga ofisi ni
 200,000×6months
=1,200,000.

Then, 1.2M÷4 = 300k

So kila mtu anatafuta 300k kwa miezi 6. Then Kila mwezi mkawe na service charge 30k umeme, internet na ulinzi, taka n.k

Umeona ilivo rahisi?

Vijana mkiwa mnasubiri kupata pesa za ofisi ambapo ni gharama sana, kwanini msichangie afu muingie na kufanya mapambano kwa njia hii?

Then mkishakuwa, kila mtu akapambane zake.

I think it can work fully.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni