Powered By Blogger

Jumatano, 20 Novemba 2013

SHERIA ZA AJIRA KWA WATOTO (TANZANIA)

Ajira kwa Watoto

Je Sheria za kazi zinamuelezea vipi mtoto?
Kifungu cha 4 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka, 2004 kinamuelezea mtoto kama mtu mwenye umri chini ya miaka 14 isipokuwa kwa ajira zilizo katika sekta hatarishi,  mtoto maana yake ni mtu mwenye umri wa chini ya miaka 18.
Je kuna sheria yeyote inayosimamia ajira kwa watoto?
Ndio, kuna sheria kadha wa kadha zinazoelezea ajira kwa watoto kama vile katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, sheria ya Watoto na sheria ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi zikiwa ni miongoni mwa nyingi. Lakini linapokuja suala la ajira na kazi, Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004 ndio inayokidhi hasa.
Je kuajiri mtoto inakubalika kisheria?
Kwa ufupi sheria inakataza mtoto mwenye umri chini ya miaka 14 kuajiriwa. Sheria pia inaendelea kukataza ajira kwa watoto chini ya miaka 18 katika maeneo ya migodi, viwanda, kama mabaharia katika meli au kazi nyingine yeyote inayotambulika kua hatarishi. Hata hivyo, sheria inaruhusu ajira kwa watoto wa miaka 14 katika kazi nyepesi ambazo sio hatarishi kwa afya ya watoto na maendeleo na haihatarishi mahudhurio ya watoto shuleni, ,mafunzoni au programu za kujifunza. Kwa ujumla ustawi wa watoto hautakiwi kuhatarishwa hata kidogo.
Je kuna adhabu kwa mtu atakayeajiri watoto kinyume cha Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004?
Ni kosa kuajiri watoto kinyume na sheria ya kazi inavyosema na adhabu inatolewa chini ya kifungu cha 102 (2) ambacho kinampaHakimu wa Wilaya na Mkazi kutoa adhabu sawa na faini isiyozidi shilingi milioni 5 au kifungo cha mwaka mmoja au vyote faini na kifungo kama mahakama itavyoona inafaa, kutegemea na mazingira ya kesi yenyewe.

Ni vipi Waajiri watafahamu kua maeneo yao ya kazi ni hatarishi?
Sheria inamtaka Waziri kuandaa orodha ya sekta hatarishi na kuisambaza kwa umma. Kwa sasa kuna rasimu ya orodha hiyo kutoka kwa Waziri wa Kazi na Ajira lakini bado haijasambazwa na kua rasmi.
Je mwajiri atakua na makosa kwa kuajiri mtoto kwa kupewa taarifa zisizo sahihi au kutotambua?
Kama mwajiri atatoa madai kwamba hakufahamu kwamba mtu aliyemuajiri ni mtoto wakati wa kumpa ajira au kudai kupewa taarifa zisizo sahihi watakua na wajibu wa kuthibitisha kua ilikua sahihi kwa wao au mtu mwingine yeyote mwenye akili timamu kuamini kwamba mtoto huyo  alikua na umri wa kuajiriwa. Ni lazima waonyeshe kwamba kulikua na hatua za kutosha kuhakikisha hawaajiri watoto. Uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa, kumbukumbu za usahili na wazazi wa mtoto na uthibitisho mwingine wowote kuonyesha kwamba walipotoshwa, hii itawasaidia kuwaepusha na adhabu iliyotajwa hapo juu.
Je mtu atakua na makosa kwa kukuwadia mtoto kwa ajira?
Sheria inakataza kuajiri mtoto na kukuwadia mtoto kwa ajira. Kama kutakua na uthibitisho kwamba kulikua na ukuwadi wa watoto kwa ajira basi mtu huyo atakua na makosa na atachukuliwa hatua sawa na Yule aliyeajiri mtoto au watoto katika maeneo yake ya kazi.

KWANINI WAFANYWE WATUMWA....??? hawajaomba hawa kuletwa duniani......

Hiii inaonesha wazi vipi watoto wadogo chini ya miaka 10 wanavyotumwa kama punda, au zaidi ya punda katka Siku za kazi.... Ujenzi Sio kazi ya kufanyishwa mtoto waiaka 9, kubebeshwa Vkarai vya zege ni kumuua kiakili pamoja na kuzorotesha maendeleo yake ya kimwili.....
Mashirika ya kusaidia na kutetea haki za watoto yako Wapi..???
MNASHAURI nini wenzangu katika hiliii maana tunawaumiza watoto, Sio kosa Lao wao kuja duniani jamani ni kazi matunda ya kazi ya wazazi wao.....

Jumanne, 5 Novemba 2013

BAADHI YA ATHARI ZA KAZI (ajira) ZA UTOTONI

"..........Tushukuru wazazi wetu kupata uwezo wa kutusomesha, tujifunze ili tuwe mfano kwa jamii....."






kama watoto kama hawa wangesomeshwa, wangewezeshwahaya yote yasingekuwepo......


fungua hiii link uone ILO ilivyowezakufafanua kwa usahihi hali inavyokuwa  www.ilo.org/public/english/bureau/inf/wdacl/kiswahili.htm  



Jumamosi, 2 Novemba 2013

TUKIWAWEZESHA WANAFUNZI WANAFAULU....................................................... BIG UP

 Matokeo ya Darasa la saba mwaka 2013 yametangazwa

Matokeo ya darasa la saba mwaka 2013 yametangazwa na mwaka huu ufaulu umeongezeka toka asilimia 30.72 mwaka jana na kufikia asilimia 50.61 mwaka huu.

Kaimu katibu mtendaji wa baraza la mitihani, Charles Msonde amesema jumla ya watahiniwa 427,606 kati ya 844,938 wamefaulu mtihani kwa kupata alama zaidi ya 100 katika jumla ya alama 250.

Watahiniwa wamefaulu zaidi somo la kiswahili kwa asilimia 69.06 na somo ambalo wamefaulu kwa kiwango cha chini ni hisabati maana ufaulu wake ni asilimia 28.62

Ijumaa, 1 Novemba 2013

MOVIE TIMEEEE.................






movie gani kwa sasa ya watoto unapenda kuiangalia or unawish japo siku moja utaingali (kwa mara ya kwanza au zaidi na hapo)



TUKUMBUSHANE KWENYE COMMENTS WW HUWA UNAPENDA MOVIE IPI?

JARIBU HIII KWA MTOTO WAKOOO AU WEWE MWENYEWE... HOW SCINCE WORKS



Here's a fun scientific “interaction” that your child can perform using basic materials found in the kitchen. And, as an added bonus, performing it for your family will help to boost your child's confidence, and make your countertenor shine!

What You Need:

  • Empty cup
  • 1 teaspoon baking soda
  • 2 teaspoons liquid dish detergent
  • Measuring spoon
  • Plastic spoon or straw for stirring
  • Fresh lemons, sliced into quarters
  • Wet and dry paper towels

What You Do:

  1. In advance, have your child prepare his cup full of special ingredients. Place the baking soda and liquid dish detergent in the empty cup and stir to mix.
  2. Now it’s time for the show to begin.  Gather your family—the audience—in the kitchen for the show. For best results, do this performance over a counter that could use a gentle cleaning. 
  3. Have your child begin the show by introducing himself, telling the audience that he can create a cleaning concoction from lemons. He may wish to add a little drama to his presentation by wearing a white jacket (to resemble a lab coat) or putting on safety glasses.
  4. Have him squeeze the juice of two quarters of a lemon into the cup.
  5. When the lemon juice mixes with the baking soda and dish soap, it begins foaming immediately, creating a fluffy pile of lemon-scented suds!
  6. Your child can actually use these suds to clean the counter. Have him simply dump the suds onto the countertop, and use a paper towel to wipe the suds across the counter. Follow up with a wet paper towel to remove any baking soda residue.
What Happened? The acid in the lemons interacted with the baking soda, which is a base. The interaction created carbon dioxide bubbles, which made the soap get bubbly and sudsy. Be sure to explain the "why" behind this interaction to your child prior to the show, so he can answer any questions generated by the audience!

TEACHING CHILDREN THROUGH WORK AND PLAY

TEACHING CHILDREN THROUGH WORK AND PLAY


We have learned so much recently about the importance of play for young children that many families may overlook how meaningful work can also nurture development.
Young children flourish when allowed to enter the world of real work that surrounds them - from picking up toys or feeding the cat to grating carrots for salad. In the company of family or other adults, children eagerly engage in work. They want to 'help' with the pursuits of adults, and this work can be a crucial part of their early learning.
If you shield young children from a whole category of activity simply because it is called 'work' and not 'play,' you may be limiting their developmental opportunities.
On the other hand, if you invite children to participate in work andplay, you give them many more ways to grow and learn.
Through work that is meaningful and a real contribution to the family or group, even young children can gain a sense of purpose, and come to feel more a part of the family.
With proper adult supervision, there are many types of chores that families can consider for young children, which can help them begin learning about responsibility, independence and caring for themselves. Here are a few examples:
  • Gathering, preparing, and cooking food Even when they are too young to help with lunch or dinner, children can play a role in preparing snacks. And by taking your children to the grocery or market, you can help them better understand where food comes from and how we buy it.
  • Running errands 
    Letting young children run errands conveys your feelings of trust in them. When you need something - another family member or the phone or a sponge - tell one of your children you need help.
  • Caring for younger children 
    Even simple tasks (like reading or singing to younger family members) help older children learn about responsibility and sharing.
  • Housekeeping 
    Children can help set the table and serve themselves at meals. If you are vacuuming the carpet, you can empower your child by letting him run this most-adult-of-all housekeeping tool.
  • Caring for animals 
    Pets and livestock require water, food and clean environments. Young children can learn valuable lessons by caring for animals.
  • Gardening 
    Nurturing plants helps children learn about the wonders of nature. If you don't have space for a garden, a small window planter can bring opportunities to explore.
In all of these activities, it's important to remember several points:
  • Keep in mind what your children can accomplish, and how much you need to supervise to make sure the activity is safe.
  • Even young children can tell the difference between busy work and real work.
  • Also, remember that many chores actually take longer with the help of young children, but a little patience and a few extra minutes lets them reap real benefits from assisting the family.
By matching your expectations to their abilities, encouraging and approving their efforts, and allowing plenty of time for the performance of each task, you can give your young children many opportunities to learn and grow through work.
Excerpted from "More Than Line Leader and Door Holder: Engaging Young Children in Real Work," by Christine A. Readdick and Kathy Douglas - an article in the NAEYC journal, Young Children.

READ CAREFUL....... WAIT FOR THE COMMENT

PRE-PRIMARY AND PRIMARY EDUCATION UNIT| Print |
Objective
To create a conducive environment for provision of quality pre- primary and primary education.

This Unit will perform the following activities:-
(i)    Provide inputs for development, monitoring, evaluation and review of implementation of education policies, legislations and guidelines;
(ii)  Initiate the development and review of pre-primary and primary education curriculum, instructional materials and teaching and learning methods including physical education and ICT;
(iii)   Set standards for learning, development and care for children in pre-primary and primary education and monitor and evaluate adherence;
(iv)  Set standards and provide guidelines for delivery, performance and achievement in pre-primary and primary education and monitor and evaluate their implementation;
(v)  Monitor and evaluate quality of teaching and learning processes and outputs in pre–primary and primary education and advice accordingly;
(vi)  Prepare and disseminate guidelines for identifying and nurturing gifted and talented pupils and monitor and evaluate their implementation ;
(vii) Conduct research on issues pertaining to pre-primary and primary education and advise accordingly; and
Collect, analyse, store and disseminate data on pre-primary and primary education.

NOOOOOO ZEROOOO ANYMOREEEE IN TZ

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI




UPANGAJI WA VIWANGO VYA ALAMA, MATUMIZI YA ALAMA ENDELEVU YA MWANAFUNZI NA UFAULU

1.           UTANGULIZI

Wizara imekusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne na cha Sita pamoja na Matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi (Continuous Assessment ama CA) kwa ajili ya kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi. Maoni ya wadau yamekusanywa kwa sababu kwa muda mrefu sasa upangaji wa viwango vya alama vinavyotumika na utaratibu wake katika mitihani ya kuhitimu Kidato cha Nne na Kidato cha Sita umekuwa haufanani pamoja na kwamba mitihani hiyo yote ni ya elimu ya sekondari. Pia mfumo masuala mbalimbali ya mitihani katika elimu ya sekondari umekuwa na miundo tofauti ikiwemo ule unaotumika shuleni na ule wa Baraza la Mitihani la Taifa. Kwa sasa kuna miundo mikuu miwili katika mfumo huo.

Muundo wa Kwanza ni upangaji wa viwango katika ngazi ya Shule ambapo Alama Mgando (Fixed Grade
Ranges) zifuatazo hutumika kupanga madaraja: A = 81 – 100; B = 61 – 80; C = 41 – 60; D = 21 – 40 na F = 0
– 20. Muundo huu umetumika kwa muda mrefu na umezoeleka kwa walimu na wanafunzi wa elimu ya
sekondari kwa ujumla.

Muundo wa Pili ni wa viwango vinavyotumiwa na Baraza la Mitihani la Taifa ambapo ambapo kabla ya mwaka 2012 muundo wa viwango nyumbufu (flexible grade ranges) ulitumika. Katika muundo huu uwigo wa alama ulibadilika badilika kulingana na hali ya matokeo ilivyokuwa kwa mwaka husika. Lakini kuanzia mwaka 2012, Serikali iliamua kutumia mfumo wa Upangaji wa Alama Mgando (Fixed Grade Range) kwa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita. Katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 Baraza lilitumia mfumo huu wa alama mgando ambapo: A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49, F = 0 – 34. Kwa upande wa Kidato cha Sita Baraza lilitumia mfumo wa A = 80 – 100; B = 75 - 79; C = 65 – 74; D = 55 – 64; E
= 45 – 54; S = 40 – 44 na F = 0 – 39. Mifumo hii ya Baraza haikuwa inafahamika kwa wadau na hivyo kuwa sehemu ya malalamiko katika sekta ya elimu na mafunzo.

Vilevile, Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 imeelekeza kwamba katika kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi wa elimu ya sekondari, Alama za CA zitachangia asilimia hamsini (50%) na Mtihani wa mwisho utachangia asilimia hamsini (50%). Kwa upande wa Zanzibar, CA zimekuwa zikiandaliwa kwa mfumo wa asilimia arobaini (40%) na mtihani wa mwisho asilimia sitini (60%). Pamoja na kwamba Baraza halijawahi kuutumia mifumo hii tangu ilipowekwa, kumekuwa na mitazamo, maoni  na mapendekezo tofauti katika muundo na matumizi ya alama za CA. Kuna mawazo pia kwamba mfumo wa CA kuchangia matokeo ya mwisho ya mwanafunzi pia utumike kwa watahiniwa wa kujitegemea (private candidates). Kwa sasa matokeo ya mitihani ya watahiniwa hawa yamekuwa yakitumia alama za mtihani wa mwisho tu na hivyo kutafsiriwa kama utaratibu ambao unamwonea mwanafunzi ambaye anahamu ya kujiendeleza kielimu lakini anakwama kwa sababu mfumo unaotumika siyo rafiki kwa mtahiniwa.

Kwa mantiki hii, Wizara imedhamiria kufanya harmonization ya masuala ya alama katika mitihani ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita ili kupata muundo mmoja na ulio wazi kwa wadau wote wa elimu ya sekondari. Lakini  pia  serikali  imedhamiria  kuhakikisha  tathmini  za  wanafunzi  katika  ngazi  mbalimbali zinakwenda sambamba na matarajio ya mitaala inayotumika na ambayo inahuishwa mara kwa mara ili iendane na wakati na mahitaji ya elimu katika ngazi mbalimbali.



1
2.           DHANA YA MITIHANI NA ALAMA

Mitihani hutumika kwa madhumuni mbalimbali ikiwemo kupima endapo malengo ya kujifunza na kufundisha yamefikiwa na pia kubaini changamoto mbalimbali katika utoaji wa elimu katika ngazi husika. Kimsingi, mfumo wa mitihani ni jambo linalopangwa kwa kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo hali halisi ya elimu katika ngazi husika. Mfumo unaweza kubadilika kulingana na elimu inavyoendelea kukua na mahitaji mbalimbali yanavyoendelea kujitokeza. Mtihani wowote lazima uwe na matokeo. Ili matokeo haya yapatikane, kila nchi imejiwekea utaratibu wa kuyapata matokeo hayo kulingana na malengo (objectives) ya mtihani husika.

Kitaalamu, mtihani una uhusiano mkubwa sana na mitaala (curricula) na mihtasari yake na jinsi mitaala hiyo inavyofundishwa na wanafunzi kujifunza (curricula instruction or delivery). Mitihani pia huwa inafanyika katika muda maalum na kwa hivyo kuna:

a)           mitihani kwa ajili ya kupanga wanafunzi katika makundi (streams) kulingana na umahiri wao (placement assessment),

b)          mitihani  ya  kubaini  kama  ufundishaji  unakwenda  vizuri  na  changamoto  zilizopo  ili kuchukua hatua rekebu kadri mwanafunzi anavyoendelea kukua kielimu (diagnostic assessment),

c)           mitihani ya kubaini ukuaji wa mwanafunzi kielimu (formative assessment) na d)          mitihani ya kumaliza elimu katika ngazi husika (summative assessment).
Mara nyingi mitihani ya kundi (a) mpaka (c) inaunda kundi la CA wakati ile ya kundi (d) inaunda kundi la mtihani wa mwisho (final examination ama FE).

Ili upimaji ufanyike, ni lazima mtihani uwe na muundo stahiki wa alama (grading structure). Muundo huu hupangwa kulingana na maamuzi ya uwigo gani utumike. Kwa mfano, ngazi nyingi za elimu hutumia uwigo wa alama 0 hadi 100 na kuna sehemu nyingine uwigo wake ni 0 hadi 50. Kwa miaka mingi, uwigo wa alama kwa Kidato cha Kwanza hadi cha Sita hapa nchini umekuwa wa alama 0 hadi 100.

Pia, kimsingi, kuna mifumo miwili ya upangaji wa viwango vya ufaulu duniani katika kutunuku ufaulu. Baadhi ya nchi au mifumo hutumia viwango vinavyobadilika (flexible grade ranges) ambavyo hupangwa kwa  kutegemeana  na  ufaulu  wa  watahiniwa  katika  somo  husika.  Nchi  au  mifumo  mingine  hutumia viwango visivyobadilika (fixed grade ranges) ambavyo hupangwa na nchi au mifumo husika vitumike kama kipimo cha ufaulu kwa masomo mbalimbali.

Katika mitihani ya elimu  ya sekondari, Tanzania ilifuata mfumo wa kutumia viwango vinavyobadilika (Flexible Grades) kuanzia mwaka 1973 hadi 2011. Hata hivyo, kwa madhumuni ya kuwawezesha wadau kujua viwango vya ufaulu vinavyotumika katika kutunuku matokeo ya mitihani ya taifa ya sekondari, Serikali iliamua kuanza kutumika kwa utaratibu wa viwango vya ufaulu visivyobadilika (Fixed Grades) kuanzia mwaka 2012. Suala kubwa lililokuwa limebaki lilikuwa ushirikishwaji wa wadau ili kuliweka wazi suala hili na kila mdau aweze kujua mfumo na miundo yake ikiwemo mfiko wa alama na maana yake katika kila kundi la alama.

3.           MAONI YA WADAU

Kabla ya kuwashirikisha wadau, Wizara iliunda Kamati ndogo kupitia taarifa mbalimbali na kutoa mapendekezo ya jinsi muundo wa alama katika mitihani ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita unavyoweza kuwa. Kamati hii ilifanya kazi hiyo na kutoa mapendekezo yake ambayo nayo yalipelekwa kwa wadau kwa ajili ya majadiliano zaidi. Wadau mbalimbali walishirikishwa katika kutoa maoni juu ya utaratibu mpya wa upangaji wa viwango vya alama na ufaulu.  Wadau hao ni pamoja na jukwaa la taasisi za elimu ya juu, chama  cha wakuu  wa shule za  Sekondari nchini (TAHOSSA)  wakuu  wa  vyuo vya  ualimu vya umma, wamiliki na wakuu wa shule na vyuo visivyo vya Serikali (TAMONGSCO), wakaguzi wa shule kanda, muungano wa wanafunzi wa Taasisi za elimu ya juu nchini (TAHLISO), viongozi wa Wizara ya Elimu na



2
Mafunzo ya Amali Zanzibar, walimu, wanafunzi, wazazi, maafisa elimu Mkoa, Wilaya pamoja na maafisa taaluma wao, wadau kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wanataaluma na Wanasiasa.

Maoni hayo yalikusanywa kupitia mikutano mbalimbali na kwa njia ya madodoso. Wadau wote walikubaliana kwamba mfumo nyumbufu wa alama siyo mzuri na hivyo taifa lihamie kwenye mfumo wa alama mgando katika mitihani mbalimbali.

Kwa jumla wadau walipendelea utaratibu wa upangaji makundi ya alama kwa kuzingatia muachano wa alama  kumi  kumi  kutoka kundi  moja  hadi  jingine. Hali  hii  inasaidia  kuondokana  na  muundo  ambao unawalundika wanafunzi wengi na mara nyingi wasiofanana katika uwezo wao kielimu katika kundi moja. Aidha wadau walipendekeza kiwango cha chini cha ufaulu mzuri kuwa Cna hii iwe sawa na alama 40.

Kwa upande wa alama endelevu, wadau pia walipendelea kuwa CA ichangie asilimia 40 katika matokeo ya mitihani ya kuhitimu ngazi husika ya masomo. Hata hivyo, wadau walitoa angalizo kwamba ni vyema kukawa na muundo na utaratibu mzuri wa kuzipata alama endelevu za mwanafunzi. Muundo na utaratibu huo  unaweza  kutumia  mitihani  ya  Kidato  cha  Pili  na  ile ya  mock  ya  Kidato  cha  Nne ambayo  huwa inaandaliwa, kusimamiwa na kusahihishwa kwa umakini na weledi wa kutosha. Pia mwalimu naye asinyimwe fursa ya kuchangia kwenye alama za maendeleo ya mwanafunzi na hivyo matokeo ya mitihani ya muhula wa kwanza na wa pili ya Kidato cha Tatu nayo yanaweza kutumika kama sehemu ya alama endelevu. Hatua kali zichukuliwe kwa mtu na taasisi yoyote itakayobainika kukiuka maadili katika usimamiaji na uwasilishaji wa matokeo ya mitihani.

Ili kuwaimarisha wanafunzi katika tasnia ya kufikiri na kuandika, kila mwanafunzi afanye project na matokeo yake yatumike kwenye alama endelevu.  Projects hizi zianze kuandaliwa wakati mwanafunzi akiwa Kidato cha Tatu na kukamilishwa katika muhula wa kwanza Kidato cha Nne.

Kuhusu muundo wa madaraja, wadau wengi walishauri muundo uliopo sasa wa madaraja uimarishwe ili kuanza kutumia muundo wa wastani wa alama katika ufaulu (Grade Point Average ama GPA). Muundo huu huwa ni rahisi kueleweka na kuuandaa kuliko muundo wa madaraja. Lakini pia, kwa kutumia muundo wa GPA inakuwa rahisi katika kukadiria uwezo wa mwanafunzi kielimu na kufanya maamuzi mbalimbali ikiwemo kuendelea na masomo katika ngazi mbalimbali za elimu.

Mwisho, wadau walikubalianana pendekezo la muundo wa alama lijaribiwe katika mfumo halisi (actual testing) ili kujua faida na athari zake katika mfumo wa elimu kama pendekezo hilo likitekelezwa. Matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2012 na Kidato cha Sita mwaka 2013 yatumike katika kufanya majaribio na hivyo wataalamu wa mifumo wa NECTA wafanye kazi hiyo na kuleta mapendekezo yao kabla ya uamuzi wa mwisho kufikiwa. Hili lilifanyika (angalia Kiambatansho A Jedwali la 3 na la 4).

Baada ya  majumuisho ya uchambuzi wa maoni ya wadau, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Wizara ya Elimu na   Mafunzo ya Amali na Ofisi ya Waziri Mkuu  -TAMISEMI walikutana na kushauriana nini kifanyike katika kupanga    viwango    vya  alama  za mitihani  na  ufaulu.  Katika kikao  hicho,    Mawaziri, Makatibu Wakuu wa Wizara hizo na Kamishna wa Elimu, walipata nafasi ya kupitia maoni ya wadau, kujadili na kupendekeza viwango vipya vya alama za ufaulu vitakavyotumika katika mitihani ya Kidato cha Nne ya mwaka 2013 na Kidato cha Sita ya mwaka 2014. Viwango vilivyopendekezwa  vilizingatia pia maoni yaliyotolewa na wadau hapo juu na hivyo kuridhia kwamba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi sasa itangaze utaratibu wa alama za mitihani ya taifa kwa Kidato cha Nne mwaka 2013 na Kidato cha Sita kuanzia mwaka 2014.



4.           VIWANGO  NA  UTARATIBU  KUANZIA  MWAKA  2013  KWA  KIDATO  CHA  NNE  NA  MWAKA  2014
KIDATO CHA SITA

Baada ya kufanya tathmini ya maoni mbalimbali ya wadau, misingi ifuatayo ilizingatiwa katika maamuzi kuhusu makundi ya alama na muachano wake:




3
a)   Alama zitakazotumika zitakuwa A, B, C, D, E na F. Muachano wa alama kati ya kundi moja hadi jingine utafanana, isipokuwa tu pale ambapo itaonekana kuna sababu na hakuna athari za kuwa na muachano tofauti na ule ambao umetumika katika makundi mengine.

b)   Makundi ya alama hayatakuwa na clusters isipokuwa pale ambapo itaonekana kufanya hivyo kunaleta tija katika kupata picha ya wahitimu kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Kwa mantiki hii

(i)          makundi ya alama A, C, D, E na F yabaki na cluster moja moja bali kundi la alama B litakuwa na clusters mbili. Kundi la kwanza litakuwa la wale ambao wamepata alama kati ya 50 mpaka 59 na litaitwa B na lingine litakuwa la wale ambao wamevuka uwigo wa 50 hadi 59 na kuelekea uwigo wa 60 hadi 74 na hili litaitwa B+ (angalia jedwali hapo chini).
(ii)         Pamoja na kuwa na muachano wa alama 26 kama jedwali linavyoonesha hapo chini, alama A kwa miaka mingi imekuwa ikianzia alama 75 hadi 100 na kwamba pamoja na uwigo huo bado wanaofaulu kwa kiwango hicho ni wachache sana. Kwa mantiki hii, hakuna haja ya kubadilisha uwigo ila juhudi ziendelee katika ufundishaji na ujifunzaji ili kiwango cha ufaulu kiongezeke na kupata wanafunzi wengi zaidi wanaofaulu katika kundi hili.
(iii)        Pia, pamoja na kuwa na muachano wa alama 20 kama jedwali linavyoonesha hapo chini kwa miaka mingi, huko shuleni mwanafunzi aliyepata alama 21 na hadi 30 alihesabiwa kuwa na ufaulu wa chini kabisa au hafifu kwa kiwango cha alama D na ingawa ilikubalika ufaulu wa aina hiyo kwa mazingira ya nchi yetu unaridhisha. Alama F ilikuwa ni kwa wale waliopata chini ya hapo. Hivyo, alama F itaendelea kuwepo na itaanzia alama 0 hadi 19 na E itaanzia alama 20 hadi 29 na D – 30 -39. Lengo la muundo huu ni kuwa alama mbalimbali, isipokuwa kwa makundi machache, zianzie kwenye 0 yaani 0, 10, 20, 30, 40 na kuendelea badala ya kuanzia kwenye moja yaani 1, 11, 21, 31, 41 na kuendelea. Hii ni kwa ajili ya kuleta mtizamo unaofanana katika ngazi mbalimbali za elimu ambapo kwa sasa ngazi ambazo siyo za elimu msingi na sekondari zinatumia muundo wa kuanzia kwenye 0 badala ya 1.
c)    Uwigo wa jumla wa alama kwa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita utaendelea kuwa wa alama 0 hadi 100 na kila kundi katika uwigo huu limepewa tafsiri kwa ajili ya kuamua mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya mwanafunzi kulingana na malengo ya mtihani husika. Kimsingi, tafsiri zifuatazo zitakatumika
(i)          Alama  A   itakuwa  na  maana  ya  ufaulu  uliojipambanua  (distincion  or  outstanding
performance),
(ii)         Alama B+ itakuwa na maana ya ufaulu bora sana (excellent performance), (iii)        Alama B itakuwa na maana ya ufaulu mzuri sana ( very good perfomance), (iv)        Alama C itakuwa na maana ya ufaulu mzuri (good performance);
(v)         Alama D itakuwa na maana ya ufaulu wa wastani (low performance), (vi)        Alama E itakuwa na maana ya ufaulu hafifu (very low performance), na
(vii)       Alama F itakuwa na maana ya ufaulu usioridhisha (unsatisfactory performance). Wataalamu  katika  maeneo  mbalimbali  ya  elimu  na  ulimwengu  wa  kazi,  kwa  kushirikiana  na Wizara, watatoa maana ya tafsiri hizi kiutendaji katika maeneo yao kulingana pia na mahitaji yao.
d)   Alama C iwe ndiyo alama ya ufaulu mzuri ambao hauhitaji urekebu wa lazima, wakati alama D na
E ni alama za ufaulu unaohitaji urekebu kadri mwanafunzi atakavyokuwa anaendelea na masomo ili kuthibitisha kama mlengwa anaweza na kulingana na mahitaji ya eneo husika (targeted remediation). Alama F iwe alama ya eneo linalohitaji urekebu wa hali ya juu (intesive remediation) ili   mwanafunzi   huyo   aweze   kumudu   masomo   kadri   anavyoendelea   kukua   kielimu   ama atakapoingia katika ulimwengu wa kazi.

e)   Makundi ya alama yatajumuisha CA kwa kiwango cha asilimia isiyozidi 40 na mtihani wa mwisho kwa asilimia isiyozidi 60 kwa makundi yote ya watahiniwa ikiwemo wale wa kujitegemea (private





4
candidates). Hii ni kwa kuzingatia kwamba CA siyo vizuri izidi uwigo wa alama ya ufaulu mzuri unapoanzia ambayo ni C au 40.

f)    CA kwa upande wa Kidato cha Nne zitokane na mtihani wa Kidato cha Pili (alama 15), matokeo ya
Kidato  cha Tatu (alama 5 kwa kila muhula, na hivyo jumla ya alama 10), mtihani wa Mock (alama
10) na kazi mradi  au Projects (alama 5). Kwa upande wa Kidato cha Sita, CA iendelee kutokana na muundo unaotumika sasa.

g)   CA zitumike pia kwa watahiniwa wa kujitegemea. Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegmea ambao wanarudia Mitihani, CA zao  zitumike zile zilizotumika kutoa matokeo yake ya mitihani ya awali.  Kwa watahiniwa wa kujitegemea waliopitia mfumo wa Qualifying Test (QT), matokeo ya QT yatumike kama CA na mtihani wa mwisho uchangie alama 60.

h) Kwa vile alama endelevu kwa mwaka 2013 kwa wanafunzi wa Kidato cha Nne tayari zimeshawasilishwa Baraza la Mitihani  Tanzania, alama hizo zichangie asilimia 40 katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2013.

i)    Muundo wa wastani wa alama katika ufaulu (Grade Points Average ama GPA) utaandaliwa na kuanza kutumika pale utakapokuwa tayari na wadau wataelimishwa kuhusu muundo huo ili wapate kuufahamu na manufaa yake katika elimu ya sekondari.

j)    Muundo huu mpya wa alama utatumika kwa mzunguko wa miaka minne kabla haujahuishwa tena ili kuupa muda wa kutosha kuona aina ya changamoto zinazojitokeza na jinsi ya kuzishughulikia. Aina hii ya muda itaruhusu vidato vinne vya elimu ya sekondari ya kawaida na nane ya elimu ya sekondari ya juu kupimwa. Hata hivyo, uhusihaji wa masuala ya mitihani unaweza ukafanyika iwapo matokeo ya uhuishaji wa mitaala kwa ujumla utahitaji pia eneo la mitihani liguswe na kuhuishwa pia.

Kwa mantiki hii, viwango vya alama na ufaulu ni kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 1 hapa chini:

Jedwali Na 1

MUUNDO WA ALAMA NA UFAULU

ALAMA                       UWIGO WA ALAMA        IDADI YA ALAMA                          TAFSIRI

A                                     75 - 100                              26                  Ufauli Uliojipambanua

B+                                     60 - 74                               15                  Ufaulu bora sana

B                                       50- 59                               10                  Ufaulu mzuri sana

C                                      40 - 49                               10                  Ufaulu mzuri

D                                      30 - 39                               10                  Ufaulu Hafifu

E                                      20 - 29                               10                  Ufaulu hafifu sana

F                                   0 - 19                                    20                  Ufaulu usioridhisha



Kwa aina hii ya muundo wa alama, na kwa kuwa muundo wa GPA utaanza kuandaliwa na wadau kuelimishwa kabla  haujaanza  kutumika,  katika  kipindi  hiki  mpaka  wakati  huo, muundo  wa  madaraja utakuwa kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 2 hapa chini.

Jedwali Na 2

MUUNDO WA MADARAJA

MUUNDO WA ZAMANI                       MUUNDO MPYA                                              MAELEZO POINTI               DARAJA              POINTI                DARAJA



5
7-17                1                             7-17              I                                  Kundi la ufaulu uliojipambanua na bora sana

18-21              II                             18-24            II                                 Kundi la ufaulu mzuri sana

22-25              III                            25-31            III                                Kundi la ufaulu mzuri na wa wastani

26-33              IV                           32-47            IV                                Kundi ufaulu hafifu
34-35              0                             48-49            V                                 Kundi la ufaulu usioridhisha

Wataalamu wa mifumo ya mitihani watalifanyia kazi zaidi jedwali hili la madaraja ili liweze kutumika kwa ufanisi katika kipindi hiki cha mpito.
Kwa mantiki hii, Daraja Sifuri linafutwa na kuwekwa daraja litakalojulikana kama Daraja la Tano na ambalo litakuwa ndilo la mwisho kabisa katika ufaulu.

5.           HITIMISHO

Mabadiliko haya yamefanyika ili kuendelea kuimarisha mfumo wetu wa elimu na kuweka wazi taratibu mbalimbali kwa ajili ya mitihani na masuala mengine. Yako mambo mengi mengine ambayo hayana budi kuendelea kuimarishwa ikiwemo mfumo wa mitaala, walimu, mazingira ya kujifunzia na kufundishia pamoja na vitabu na vifaa vingine muhimu katika elimu. Masuala haya yanaendelea kuangaliwa kupitia mikakati  mbalimbali  ikiwemo  mpango  wa  Matokeo  Makubwa  Sasa  ama  Big  Results  Now  (BRN). Ushirikiano wa wadau wote ili kuleta tija kwenye elimu ni muhimu sana na hivyo wizara itaendelea kuwashirikisha wadau wote kwa kadri itakavyohitajika na wadau pia wanaombwa wasiache kuishirikisha wizara pale watakapokuwa na jambo lolote ambalo linahitaji ushirikiano ili kwa pamoja tuweze kupata mafanikio katika sekta ya elimu.



Imetolewa,




KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI


Investment to future

Ideally, what should be said to every child, repeatedly, throughout his or her school life is something like this: 'You are in the process of being indoctrinated. We have not yet evolved a system of education that is not a system of indoctrination. We are sorry, but it is the best we can do. What you are being taught here is an amalgam of current prejudice and the choices of this particular culture. The slightest look at history will show how impermanent these must be. You are being taught by people who have been able to accommodate themselves to a regime of thought laid down by their predecessors. It is a self-perpetuating system. Those of you who are more robust and individual than others will be encouraged to leave and find ways of educating yourself — educating your own judgments  Those that stay must remember, always, and all the time, that they are being molded and patterned to fit into the narrow and particular needs of this particular society.”